JUVENTUS WATINGA KIRAHISI ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mabingwa wa Italia Juventus wametinga kirahisi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kupata ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wa marudio dhidi ya FC Porto.

Ikiwa inaongoza kwa magoli 2-0 katika mchezo wa kwanza, Juventus, ilikamilisha mambo pale, Paulo Dybala, alipofunga kwa mkwaju wa penati baada ya Maxi Periera kushika mpira na kutolewa nje.

Baada ya goli wenyeji Juventus walicheza mpira katika eneo la kati na kufanikiwa kutinga hatua nane bora kwa mara ya pili mfululizo katika mika minne.
                       Refa akimpa kadi nyekundu  Maxi Periera baada ya kuunawa mpira

         Paulo Dybala akijipinda na kupiga penati iliyozaa goli pekee katika mchezo huo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post