JUVENTUS YAIFUNGA NAPOLI KATIKA KOMBE LA KOPA ITALIA

Paulo Dybala amefunga kwa mikwaju miwili ya penati wakati Juventus ikiifunga Napoli kwa magoli 3-1 katika mchezo wao wa nusu fainali ya kwanza wa kombe la Coppa Italia.

Alikuwa Jose Callejon aliyewapatia wageni goli la kuongoza baada ya kufanya shambulizi nzuri, lakini Muargentina Dybala alisawazisha kwa mkwaju wa penati.

Gonzalo Higuain aliwafungia wenyeji goli la pili kabla ya baadaye Dybala kuongeza goli la tatu baada ya kipa Pepe Reina kumuangusha Juan Cuadrado. 
                                                      Paulo Dybala akifunga goli kwa mkwaju wa penati

                                          Gonzalo Higuain akifunga goli la pili katika mchezo huo 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post