KADA WA CHADEMA, LAWRENCE MASHA AJITOA KUWANIA URAIS TLS

Mwanasheria Lawrence Masha aliyekuwa akiwania nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amejiondoa katika nafasi hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Baada ya kujitoa ametangaza kumuunga mkono Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA,  Tundu Lissu ambaye naye ni miongoni mwa wagombea wa urais wa TLS.
Mwanasheria huyo amezungumza na wanasheria katika ukumbi wa mikutano wa AICC ulioko jijini Arusha jioni ya leo na kuwaomba wote waliokuwa wamepanga kumpigia kura sasa wampigie Tundu Lissu kwa anaweza na anafaa kushika nafasi hiyo.
Uchaguzi mkuu wa TLS unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Machi 18 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post