KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA SERIKALI KUWA MFANO KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL

SHARE:

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Taasisi za Serikali na Mashirika yote ya Umma kutumia kituo cha kutunzia kumbukumbu cha T...

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Taasisi za Serikali na Mashirika yote ya Umma kutumia kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Data Centre)chenye hadhi ya juu kabisa katika viwango vya ubora na usalama wa Taarifa na Kumbukumbu. Kamati pia imezitaka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia Kituo hicho katika kutunza kumbukumbu zake ili kuwa mfano kwa Taasisi nyingine za Umma.

Akizungumza katiko maazimio ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mara baada ya ziara ya siku moja ya Kamati hiyo kuitembelea Kampuni ya Simu Tanzania TTCL pamoja na miradi ya Mkongo wa Taifa na Kituo Mahiri cha kutunzia kumbukumbu (Data Centre), Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Norman Sigala amesema, uhai wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL upo mikononi mwa Serikali ambayo ina jukumu kubwa la kuihusiha Kampuni hiyo yenye uwekezaji mkubwa.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imezitaka Taasisi zote za Umma na binafsi kulipa madeni zinazodaiwa na TTCL kuiwezesha Kampuni hiyo kujiendesha kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na Watendaji wa Umma wanaogharamiwa huduma za Mawasiliano kutumia huduma za simu za TTCL katika maeneo yote yenye huduma hizo.

Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe Rita Kabati amesema, kukamilika kwa Mchakato wa kuondoka kwa Bharti Airtel ndani ya TTCL kunahitaji kwenda sambamba na uwezeshaji wa mtaji kama ilivyofanyika kwa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambazo sasa zinafanya vizuri.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Prof. Norman Sigala na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kushoto).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kulia) alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Mhandisi Dk. Marry Sassabo akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya maswali yalioulizwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kampuni ya TTCL.
Meneja Mtandao wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Amani Kichele (wa pili kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali ya Mkongo wa Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kampuni ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.
 
Awali akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba amesema, ushirikiano mkubwa uliotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu umewezesha Serikali kuchukua hatua ambazo zimeipa TTCL nguvu mpya ya kurejea katika nafasi yake ya kihistoria ya kuwa Kinara wa utoaji huduma za Mawasiliao nchini.

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na Serikali kulipa sh Bilioni 14.7 na kuhitimisha ubia usioridhisha wa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL uliodumu kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu bila kuleta tija iliyotarajiwa. Hatua nyingine ni pamoja na Serikali kuiruhusu TTCL kutumia majengo yake kama dhamana kuweza kupata mikopo ya Shilingi bilioni 96.6 kwa ajili ya uwekezaji, kurekebisha mizania ya Kampuni kwa kufuta madeni ya takribani Shilingi bilioni 100 hivyo kufanya Kampuni kuweza kukopesheka.

Maamuzi mengine ni Serikali kuipatia TTCL masafa ya Megahezi 1800 na 2100 ambayo yametumika kufunga mitambo ya mawasiliano ya teknolojia za 2G (GSM), 3G (UMTS) na 4G (LTE) pamoja na kuikabidhi TTCL dhamana ya kusimamia na kuendesha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano(NICTBB) na Kituo cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao (National Internet Data Centre).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mheshimiwa Omari Nundu amesema, TTCL inakabiliana na changamoto kadhaa zinazohitaji utatuzi wa haraka. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na TTCL kukosa mtaji wa kutosha( Takriban shilingi bilioni 300) kunununua teknolojia za kisasa na mitambo mipya ili kuondoa miundombinu chakavu na kuongeza ufanisi na ubora wa huduma.

Changamoto nyingine ni madeni ya ankara za huduma ambayo TTCL inadai taasisi za Umma na serikali ambayo yamefikia takribani Sh Bilioni 9 ambazo endapo zingelipwa kwa wakati, zingesaidia sana kuimarisha utendaji wa TTCL.

Nao Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja Mhe Japhari Michael na Mhe Prof Anna Tibaijuka wamesema, TTCL inao wajibu mkubwa kwa Taifa kuhakikisha kuwa Mawasiliano yanafika nchi nzima na hasa katika maeneo ya Vijijini ambako Kampuni binafsi za Mawasiliano hazitoi kipaumbele katika kufikisha huduma zake.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA SERIKALI KUWA MFANO KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL
KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA SERIKALI KUWA MFANO KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL
https://2.bp.blogspot.com/-n7N4Lc2jAvM/WNIMBevhvmI/AAAAAAAAYY0/CJadDP1h7jsVH4QprDUvIwQL0lVGah6hQCLcB/s1600/unnamed.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-n7N4Lc2jAvM/WNIMBevhvmI/AAAAAAAAYY0/CJadDP1h7jsVH4QprDUvIwQL0lVGah6hQCLcB/s72-c/unnamed.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/kamati-ya-bunge-ya-miundombinu-yaitaka.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/kamati-ya-bunge-ya-miundombinu-yaitaka.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy