KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU NYERERE

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr.Leonard Chamriho akitoa taarifa fupi ya wizara kuhusiana na ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea kuona ujenzi wa jengo hilo
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akielezea masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara kwenye jengo hilo linaloendelea kujengwa na linatarajiwa kumalizika Desemba 2017
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akisoma taarifa ya mradi wa jengo la tatu la abiria (TBIII), kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi huo
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Norman Sigalla akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakitembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Mbunge Charles Kitwanga wa kwanza kushoto akifurahia jambo na wajumbe wenzake wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, leo wakati walipotembelea jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mhandisi Angela Maeda (kulia) akitoa maelezo mbalimbali kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu leo ilipotembelea jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere
Mhandisi Mwanaidi Mkwizu aliyenyoosha kidole kuwaonesha wajumbe wakati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, majenereta ya kisasa yaliyofungwa kwa ajili ya matumizi ya jengo la tatu la abiria (TBIII) la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, walipofanya ziara. Kushoto ni Prof. Anna Tibaijuka.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara kwenye jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Mhe. Mussa Ntimizi, mbele leo akiwaongoza wajumbe wenzake wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakipita katika moja ya madaraja ya kisasa yaliyofungwa kwenye jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, walipofanya ziara leo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post