KAMPUNI YA CEICE YA CHINA KUJENGA VIWANDA ZANZIBAR

SHARE:

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya utengenezaji, usafirishaji na uagizaji wa vifaa vifav...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya utengenezaji, usafirishaji na uagizaji wa vifaa vifavyotumia mfumo wa Kisasa wa mawasiliano ya Nchini China { CEICE } ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar. Wa pili kutoka kushoto aliyevaa suti nyeusi na miwani ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CEICE Kutoka Nchini China Bwana Liu Yang
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CEICE Kutoka Nchini China Bwana Liu Yang upo akimkabidhi Balozi Seif zewadi ya Nembo ya Kampuni hiyo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya utengenezaji, usafirishaji na uagizaji wa vifaa vifavyotumia mfumo wa Kisasa wa mawasiliano ya Nchini China { CEICE } baada ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini kwake Vuga.
                                                                                                    
                                                                                              Picha na – OMPR – ZNZ.


Kampuni ya utengenezaji, usafirishaji na uagizaji wa vifaa vifavyotumia mfumo wa Kisasa wa mawasiliano ya Nchini China { CEICE } imeonyesha nia yake ya kutaka kujenga viwanda vya utengenezaji wa vifaa hivyo Visiwani Zanzibar katika azma yake ya kutoa huduma ndani ya ukanda wa Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika.

Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Kanda ya Kusini Mashariki ya Afrika Bwana Kang Kai alisema hayo wakati Ujumbe wa Viongozi Sita wa Kampuni hiyo kutoka Nchini China na Mjini Dar es salaam ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Kang Kai alisema Kampuni ya CEICE imeamua kuwekeza miradi yao Zanzibar kwa lengo la kuunga mkono mpango Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China wa kuelekeza nguvu zake za Uchumi katika kusaidia Maendeleo ya Bara la Afrika { China – Africa }.

Alisema kutokana na ongezeko kubwa la vyuo Vikuu Bara la Afrika hivi sasa linazalisha wasomi wengi ndani ya vyuo hivyo kundi ambalo linaweza kutumia taaluma yao kupitia ushirikiano na Miradi inayotekelezwa na Kampuni ya CEICE.Bwana Kang Kai alisema Kampuni ya CEICE imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa vifaa vya Kieletronik na kuviuza kwa Makapuni makubwa ya Kimataifa yakiwemo yale ya Sam sung na Sonny.

Alisema ujenzi wa Viwanda hivyo ndani ya Visiwa vya Zanzibar mbali ya kuwapatia ajira wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu lakini pia watapata fursa ya kutumia vipaji walivyonavyo katika uzalishaji ndani ya viwanda hivyo.

“ Mpango wetu wa kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar unalenga kutoa ajira pana katika miradi ya Viwanda pamoja na Umeme unaoambatana na mfumo wa kisasa wa ulinzi unaotumia umeme yaani Security System ”. Alisema Bwana Kang Kai.

Naye Mkurugenzi wa huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Nd. Shariff Shariff aliueleza Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya CEICE kwamba Serikali inahitaji Viwanda katika mpango wake wa kuelekea Nchi ya Viwanda.

Nd. Shariff alisema katika kuupa nguvu mpango huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga eneo maalum ndani ya Ukanda wa Maeneo huru ya Uchumi yaliyopo Fumba kwa ajili ya Taasisi na Kampuni zinazohitaji kutaka kujenga viwanda vyao Zanzibar.

Akitoa shukrani zake kwa Ujumbe huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema zaidi ya wakaazi Milioni 600 wanaoishi ndani ya ukanda wa Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika wanahitaji huduma muhimu za mitandao ya kisasa.

Balozi Seif alisema huduma za upatikanaji wa Vifaa kama TV, Simu na hata vitu vya umeme ni sehemu ya maisha kwa sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uliopo hivi sasa unaoifanya Dunia kuonekana kama kiganja badala ya Kijiji.

Ujumbe wa Kampuni hiyo ya utengenezaji, usafirishaji na uagizaji wa vifaa vifavyotumia mfumo wa Kisasa wa mawasiliano ya Nchini China { CEICE } ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wake Bwana Liu Yang upo Nchini Tanzania kuangalia maeneo ambayo inaweza kuwekeza miradi yao.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Kamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
6/3/2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: KAMPUNI YA CEICE YA CHINA KUJENGA VIWANDA ZANZIBAR
KAMPUNI YA CEICE YA CHINA KUJENGA VIWANDA ZANZIBAR
https://2.bp.blogspot.com/-zqmau8QA0go/WL3kxd_RCEI/AAAAAAAAXgU/G7asyYdw_3g9tYlWkoEU4GkE4wUjGVZcACLcB/s1600/492.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-zqmau8QA0go/WL3kxd_RCEI/AAAAAAAAXgU/G7asyYdw_3g9tYlWkoEU4GkE4wUjGVZcACLcB/s72-c/492.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/kampuni-ya-ceice-ya-china-kujenga.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/kampuni-ya-ceice-ya-china-kujenga.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy