KASHFA: WAZIRI NAPE, NITAJIUZULU WAKILETA USHAHIDI MEZANI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kuwa atajiuzulu nafasi yake endapo atapelekewa ushahidi unaoonyesha kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.
Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha ITV, Waziri Nape alishangazwa na uwepo wa tuhuma kuwa anauhusiano wa kimapenzi na baadhi ya wasanii wa kike nchini.
“Kama mtu ana ushahidi alete hapa mezani, aseme Nape hili unalolifanya unafanya kwa sababu unauhusiano na fulani. Na mtu akileta najiuzulu uwaziri.” Alisema Waziri Nape
Waziri Nape aliwakosoa wote wanaoeneza taarifa hizo na kusema ni watu waliokosa kazi na wamekosa hoja ya kuzungumza.
Kauli hii ya Nape inakuja takribani wiki tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudai kuwa kuna baadhi ya watu wanalalamika kwa sababu tumewagusa wapenzi wao. Makonda aliyasema hayo baada ya kukosolewa na baadhi ya wananchi na viongozi akiwemo Waziri Nape kuhusu utajaji wa majina ya wasanii akiwatuhumu kujihusisha na biashara ya dawa z akulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari katika awamu ya pili ya utangazaji majina ya watuhumiwa, Makonda hakutaja majina ya anaodai kuwa walikuwa wakiumia sababu wapenzi wao wameguswa. Alisema “Wengine wanaumia tunagusa wapenzi wao, wawasaidie waache si kupiga kelele tu, ujumbe umefika.”
Awali Waziri Nape alikuwa ametoa maoni yake akiwazungumzia wasanii kama waziri mwenye dhamana ambapo alisema kuwataja wasanii hadharani bila ushahidi ni kuwaharibia majina ‘brand’ yao ambayo wameitengeneza kwa miaka mingi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post