KAULI YA KWANZA YA NAPE NNAUYE BAADA YA RAIS DKT MAGUFULI KUMUONDOA UWAZIRI

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye amewataka wanachama wa CCM na watanzania kwa ujumla kutulia kwa wakati huu kwani atakutana na waandishi wa habari na kuelezea yote haya yaliyotokea.
Mbunge Nape Nnauye ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika ujumbe unaosomeka, “Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!.”

 Kauli ya Nape inakuja muda mchache baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kumuondoa kwenye nafasi ya uwaziri aliyokuwepo na kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe kujaza nafasi hiyo.
Nafasi ya Dkt Harrison George Mwakyembe imejazwa na Prof. Palamagamba Aidan Kabudi ambao wote wanatarajia kuapishwa kesho.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post