KAULI YA MBEYA CITY KUHUSU HATMA YA MRISHO NGASSA

Weekend zilienea stori za Mrisho Ngassa anayeichezea Mbeya City ya Mbeya kuwa ataihama timu hiyo mwisho wa msimu na kurejea Oman kitendo ambacho kimezua maswali mengi kufuatia kuenea kwa taarifa, wote tunajua Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja lakini kwanini iliripotiwe kuwa ataondoka mwisho wa msimu ikiwa mkataba wake utakuwa bado haujaisha.
Mbeya City hawamuhitaji tena au wanampango wa kumuuza,  afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten  anajibu “Kitu pekee ambacho naweza kusema kwa sasa ni kwamba Ngassa ni mchezaji bado wa Mbeya Cityalijiunga na Mbeya City dirisha dogo na alisaini mkataba wa mwaka mmoja”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa December 15 2016 siku ya mwisho ya kufungwa dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017, Mbeya City walitangaza kumsajili Mrisho Ngassa kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea timu ya Fanja FC ya Oman.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post