KILICHOSABABISHA SOPHIA SIMBA NA WENZAKE KUFUKUZWA CCM

Takribani siku nne zimepita tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua maamuzi ya kuwafukuza wanachama wake kwa tuhuma za usaliti wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni mwa wanachama waliofukuzwa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Sophia Simba na Wenyeviti wa mikoa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti moja leo limetaja sababu zinazodaiwa haswaa kusababisha vigogo hao wa siasa ndani ya chama tawala kufukuzwa uanachama.
Taarifa inasema kuwa Sophia Simba yeye anadaiwa kuwa hata baada ya uchaguzi mkuu, yeye aliendelea kwenda nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA, Edward Lowassa, kwa kificho akiwa kavaa hijabu, na hivyo kudaiwa kuwa amekuwa akipeleka siri za chama kwa Lowassa.
 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
Aidha Ramadhani Madabida, yeye alifutwa uanachama kwa kutuhumiwa kumfananisha Lowassa na Mtume, jambo ambalo wajumbe walisema hilo ni kosa kubwa.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Naye Jesca Msambatavangu alifukuzwa baada ya kudaiwa kuzima jenereta wakati wa mkutano wa kampeni wa aliyekuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, huko Iringa na kusababisha Dk. Magufuli kutosikika vizuri.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
Wakati huo huo Erasto Kwilasa, alifukuzwa CCM baada ya kutuhumiwa kupeleka siri za chama Mkoa wa Shinyanga kwa mtangulizi wake, Hamis Mgeja, ambaye aliamua kuachana na chama hicho na kumfuata rafiki yake kipenzi Lowassa, ambaye alikuwa anamuunga mkono wazi wazi tangu akiwa CCM.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa.
Kadhalika, Christopher Sanya, alifukuzwa uanachama kwa tuhuma za kuwa alisusa kushiriki kampeni za Ubunge Mkoa wa Mara baada ya jina lake kukatwa wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea Ubunge ndani ya chama hicho.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post