KINYESI CHA BINADAMU CHAKUTWA NDANI YA CHUPA ZA COCA COLA

Jeshi la Polisi nchini Ireland Kaskazini wameazisha uchunguzi kufuati kile kilichodaiwa kuwa ni uwepo kinyesi cha binadamu kilichokutwa katika chupa za kuwekea soda za Coca Cola.
Shughuli katika kiwanda cha Lisburn zilivurugika baada ya mashine za kiwanda hicho kukwama kufanyakazi. Kampuni ya Coca Cola imesema kuwa imeziondoa chupa zote zilizodaiwa kukutwa na kasoro hiyo.
Aidha, kampuni hiyo imesema kuwa kasoro hiyo haiathiri kwa namna yoyote ile soda ambazo tayari zipo sokoni.
Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, LisburnKiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn
Kwa mijibu wa taarifa, chupa hizo hufika kiwanda hapo zikiwa wazi kisha hujazwa soda na ndipo hufunikwa na kuuzwa maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha kupelekwa chupa tupu katika kiwanda cha Knockmore.
“Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri bidhaa zozote zilizo sokoni.” Alisema Msemaji wa Coca Coa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post