KIONGOZI WILAYANI RUFIJI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI

Rufiji. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kifuru, Kijiji cha Ikwiriri, wilayani Rufiji, Hemed Abdallah Njiwa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Ikwiriri, Iddy Malinda amethibitisha mwili wa mwenyekiti huyo kufikishwa kituoni hapo ukiwa na jeraha kubwa mgongoni lililotokana na risasi aliyopigwa kifuani, upande wa moyo.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo pia amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu wasiojulikana walifika nyumbani kwa mwenyekiti huyo kisha kumpiga risasi na kutokomea kusikojulikana.
Habari zaidi zinadai watu hao baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote kile.
-HT @ Mwananchi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post