KOCHA WA BARCELONA ABWAGA MANYANGA

KOCHA wa Barcelona,Luis Enrique ametangaza kuwa atang'atua kuinoa timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Enrique ametangaza uwamuzi huo jana Jumatano mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuiongoza Barcelona kuifunga Sporting Gijon mabao 6-1 nyumbani Camp Nou.

Enrique amewaambia waandishi wa habari kuwa anahitaji muda wa kupumzika na kuwa karibu zaidi na familia yake.Ameongeza kuwa miaka mitatu aliyokuwa kocha wa Barcelona imemuachia kumbukumbu ambayo kamwe haitafutika maishani mwake.

Enrique alianza kuinoa Barcelona Mei,2014 akichukua nafasi ya Muargentina Gerardo Martino.Mpaka sasa Enrique amefanikiwa kuipa Barcelona mataji manane.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post