KOMBORA LILILOTAKA KULIPULIWA NA KOREA KASKAZINI LIMESHINDWA KUPAA


Wikendi, Korea Kaskazini ilitangaza kupiga hatua pakubwa katika teknolojia ya urushaji wa maroketi

Maafisa wa ulinzi wa Korea Kusini wamesema Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora lakini likafeli. Korea kaskazini ilijaribu kurusha kombora hilo angani kutoka mji wa Wonsan, pwani ya mashariki.
Haijabainika Korea Kaskazini ilijaribu kurusha makombora mangapi au yalikuwa ya aina gani. Korea Kaskazini imepigwa marufuku kufanya majaribio yoyote ya kurusha makombora au majaribio ya nyuklia na Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo, imekuwa ikifanya majaribio mara kwa mara na wataalamu wanasema hilo huenda limeisaidia kupiga hatua pakubwa katika kustawisha teknolojia yake ya makombora.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post