LEICESTER CITY YAANDIKA UKURASA MPYA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Leicester City imeandika ukurasa mwingine baada ya kubadili matokeo ya kufungwa katika mchezo wa kwanza kwa kufanikiwa kuifunga Sevilla magoli 2-0 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Leicester ilionekana kama itatolewa baada ya kufungwa magoli 2-1 Hispani katika mchezo wa kwanza na kutimuliwa kocha wao Claudio Ranieri, ambaye aliiongoza hadi kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza.

Ikiwa chini ya kocha mpya Craig Shakespeare, Leicester imebadilika na ilikuwa katika kiwango kizuri jana ambapo nahodha wao Wes Morgan aliipatia goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na kisha baadaye Marc Albrighton kufunga la pili.
                                         Beki Wes Brown akifunga goli la kwanza la Leicester City 

                                    Marc Albrighton akifunga goli la pili na kuizamisha Sevilla
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post