LEMA ATUMA UJUMBE KWA RAIS KWA KUWAITA WASALITI WABUNGE WA CCM WALIOTAKA KUMTEMBELEA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) ameonyesha kusikitishwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Magufuli kuwa baadhi ya wabunge waliokua wamepanga kwenda kumuona akiwa mahabusu, wangekuwa ni wasaliti kwa chama.
Dkt Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa kikao na wabunge wa CCM katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Nimekuwa nikielezwa kuwa baadhi mliunda kamati mkitaka kwenda kumuona Lema alipokuwa gerezani, jambo hilo ni sawa na usaliti kwa chama na viongozi wa CCM, alisema M/kiti Dkt Magufuli.
Kufuatia kauli hiyo, Mbunge Godbless Lema ameandika ujumbe huu kwa Rais Dkt Magufuli;
Mh Rais Magufuli nakusalimu.
Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.
Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia , Wachungaji , Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali , sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.
Mh Rais , nimeogopa sana kwa kauli hii yako , je Taifa linakwenda wapi , hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu , basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .
Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini ,ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa , ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa Nchi hii .
Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu , ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako .
Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako , je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako ?
Mh Rais neno la Mungu linasema , Wapendeni maadui zenu , waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu .
Mungu akubariki sana , natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi .
Godbless J Lema (MB)
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post