LIONEL MESSI ASEMA SHANGILIA YAKE HAINA UHUSIANO NA MKATABA WAKE

Nyota wa soka Lionel Messi amekanusha uvumi kuhusiana na kushangilia goli lake kwa kuonyesha ishara ya kuongea na simu katika mchezo na Celta Vigo kuwa inauhusiano na suala la mkataba wake na Barcelona.

Messi alionyesha ishara hiyo jumamosi usiku wakati alipofunga goli la kwanza katika ushindi wa Barcelona wa magoli 5-0 dhidi ya Celta Vigo, hali iliyotafsiriwa kuwa anaieleza Barcelona mbona ipo kimya kuhusu mkataba wake.

Messi amesema alimfanyia ishara hiyo binamu yake aliyekuwamo uwanjani katika kundi la mashabiki wa Barcelona wakati wa mchezo huo ili kumzawadia goli hilo.

   Lionel Messi akinyoosha mkono jukwaani kumzawadia goli alilofunga binamu yake
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post