LISSU ASHINDA URAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA

Mbunge wa Singida Mashariki  na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameshinda nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyia (TLS).

Uchaguzi Mkuu wa chama hicho umefanyika leo kwenye ukumbi wa AICC  uliopo jijini Arusha ambapo Tundu Lissu ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,114 na kuwashinda wapinzani wake watatu.
Wengine waliokuwa wanagombea nafasi hiyo ni Francis Stolla aliyepata kura 64, Victoria Mandari aliyepata kura 176 na Godwin Mwapongo aliyepata kura 64. Idadi ya wapiga kura ni 1682.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TLS, Godwin Mwapongo ndiye aliyeibuka mshindi huku Baraza la Wajumbe likiundwa na Jeremiah Motebesya, Gida Lambaji, Hussein Mtembwa, Aisha Sinda, Steven Axweso, David Shilatu na Daniel Bushele.
Mgombea mmoja ambaye ni mwanachama wa CHADEMA, Lawrence Masha alitangaza kujitoa jana na kusema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu akiamini kuwa anatosha kwenye nafasi hiyo.

Uchaguzi huu umefanyika baada ya kuwa umegubikwa na mivutano mingi huku kesi mbalimbali zilikuwa zimefunguliwa mahakamani kutaka kuzuia uchaguzi usifanyike kwa madai kuwa kanuni za uchaguzi huo zina kasoro nyingi. Maamuzi ya Makama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma yaliruhusu uchaguzi ufanyike kwa kutupilia mbali kesi hizo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post