LIVERPOOL Vs ARSENAL NI VITA YA VIDUME HAWA ANFIELD LEO

LONDON, England
LEO Liverpool watakuwa nyumbani Anfield kuwakaribisha wakali wa Kaskazini mwa London, Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Kwa mara ya mwisho, timu hizo zilikutana Agosti mwaka jana kwenye Uwanja wa Emirates, ambapo Arsenal walikubali kichapo cha mabao 4-3.
Arsenal hawajaibuka na ushindi wakiwa Anfield kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne sasa.
Kuelekea mtanange wa leo, mashabiki wa soka watashuhudia vita ya wachezaji hawa watakaokuwa wakikabana koo kuzisaidia timu zao.
Sadio Mane v Kieran Gibbs
Winga Mane amekuwa silaha muhimu ya Liver na hata alipokosekana wakati wa fainali za Afcon za mwaka huu zilizofanyika Gabon, pengo lake lilionekana wazi.
Kasi na ubunifu wake utakuwa msaada mkubwa kwa Liver leo hii. Hata hivyo, atakuwa na shughuli pevu kukabiliana na beki wa kushoto wa Gunners, Gibbs.
Jumatatu ya wiki hii, Leicester walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumdhibiti Mane. Aliyefanikisha hilo ni beki Leicester, Christian Fuchs, aliyekuwa upande wa kushoto.
Gibbs atakuwa na kibarua cha kwenda sambamba na kasi ya Mane.
Joel Matip v Alexis Sanchez
Matip atalazimika kwenda hatua kwa hatua na Sanchez huku akiwa makini pia na kasi ya raia huyo wa Chile. Kwa kushirikiana na Dejan Lovren, Matip hapaswi kujisahau kwa Sanchez.
Mbali na kasi, straika huyo wa Arsenal amekuwa mwepesi mno anapokuwa katika eneo la hatari la timu pinzani.
Emre Can v Granit Xhaka
Katikati ya uwanja nako kutakuwa na vita ya viungo hao. Hata hivyo, Can ambaye amekuwa akihaha kutema cheche zake, alilazimika kuingia uwanjani katika mchezo dhidi ya Leicester baada ya kuumia kwa Jordan Henderson.
Hata hivyo, Mjerumani huyo hakuonekana kuwa na msaada wowote kikosini.
Kwa kuwa si rahisi kwa Henderson kucheza mchezo wa leo, kuna uhakika mkubwa wa Can kuingia uwanjani lakini atapaswa kuimarisha aina yake ya uchezaji.
Mwenzake Xhaka naye amekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu wake huu wa kwanza akiwa England.
Katika vita ya wawili hawa, yeyote atakayeongeza umakini atakuwa amemfunika mwenzake na kuibeba timu yake.
Roberto Firminho v Laurent Koscielny
Makali ya Mbrazil huyo katika safu ya ushambuliaji yamemfanya kuwa kipenzi cha kocha Jurgen Klopp.
Firminho amejihakikishia namba kikosini na kumsahaulisha Klopp kuhusu Divock Origi na Daniel Sturridge hata wanapokuwa si majeruhi.
Nyota huyo ameshafunga mabao nane ya ligi na anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji wenye mabao mengi katika kikosi cha Liver.
Hata hivyo, leo atakuwa akitoana jasho na Koscielny ambaye amekuwa nguzo imara na ya kuaminika kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post