LULU ATOA PUVU UCHUMBA WAKE KUVUNJIKA

JUZIKATI yaliibuka madai kwamba, uchumba wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na yule bosi wa redio Bongo umevunjika huku kila moja akiongea lake. Madai hayo yalienea kwenye mitandao ya kijamii na wapo waliokwenda mbali zaidi kudai kuwa, sasa Lulu karejea kwao na ana mpango wa kuanzisha maisha yake mengine.
“Wamemwagana, uchumba haupo tena, ila kusema ukweli inauma kuachwa na umpendaye,” aliandika mdau mmoja kwenye Mtandao wa Instagram kisha akasindikiza maneno hayo kwa picha ya Lulu na baby wake huyo.
Kufuatia madai hayo kusambaa mithili ya moto wa kifuu huku mashabiki wengi wa mastaa hao wakipiga simu kwenye chumba chetu cha habari na kutaka ufafanuzi wa habari hizo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Lulu kupitia simu yake lakini alipoulizwa, badala ya kutoa ufafanuzi alitoa povu kuashiria kuwa hataki habari zake ziandikwe.
“Sitaki kuongelea chochote…sitaki kuongelea chochote, pliz…unajua mimi siyo mtu wa magazeti kabisa na unanijua vizuri…” alisema Lulu na kumuacha mwandishi ameduwaa hasa kwa ile  sentensi kwamba eti yeye si mtu wa magazeti.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post