MADAKTARI WA KENYA WAKOMA KUAJIRIWA MAKTARI KUTOKA TANZANIA

Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, Dkt Magufuli kukubali ombi la serikali ya Kenya kupatiwa madaktari 500 ili kupunguza tatizo la matabibu nchini humo, madaktari wa nchi hiyo wamekuja juu na kupinga uamuzi huo.

Muungano  wa Madaktari Nchini Kenya (KMPDU) umepinga mpango wa serikali ya nchi hiyo kuingiza madaktari 500 kutoka Tanzania huku ikiitaka serikali kuajiri kwanza madaktari 1,400 ambao hawana ajira.

Ombi la Kenya limekuja kufuatia mgomo wa madaktari uliodumu kwa siku 100 nchini humo na kusababisha sekta ya afya kuyumba sana huku wananchi ambao hawana uwezo wa kwenda vituo binafsi wakiachwa wanateseka bila huduma za kiafya na wengine kufariki dunia.
Rais Magufuli jana alipofanya mazungumzo na Waziri wa Afya wa Kenya pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam alisema kuwa, Tanzania itapeleka madaktari hao nchini Kenya wakiwa ni wale ambao hawajaajiriwa kwa sasa.

Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tukiwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hatuwezi kuona ndugu yetu anateseka na tusimsaidie, alisema Rais Magufuli


Aidha, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema kuwa, ingekuwa vyema kama serikali ya Kenya ingemaliza migogoro yote na madaktari wa nchi hiyo ndipo wale wanaotoka Tanzania waweze kwenda na kufanya kazi nchini humo.

MAT wakitolea ufafanuzi jambo hilo wameelza, usalama wa madaktari hao utakuwa katika hatari kubwa endapo mgogoro wa madaktari wa Kenya dhidi ya serikali utaendelea.

Kwa mujibu wa tangazo la ajira lililotolewa jana na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, madaktari watakaokuwa na sifa za kuajiriwa Kenya watapewa mikataba ya miaka miwili.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post