MADHARA YATOKANAYO NA KUKAA MUDA MREFU BILA KUJAMIIANA

Kujamiiana huwasaidia watu kupunguza mawazo. Watafiti kutoka nchini Uskochi wamegundua kuwa watu ambao hawajafanya mapenzi kwa muda mrefu husumbuliwa na msongo wa mawazo hasa wanapoongea mbele ya jamii (public speeking), ukilinganisha na wale ambao wanakuwa wamefanya mapenzi/kujamiiana ndani ya muda wa wiki mbili.
Kwa wanaume, kujamiiana hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya tezi dume. Ripoti iliyowasilishwa na American Urological Association ilibaini kuwa wanaume wanaojamiiana mara nyingi huwa na furaha na pia kwa asilimia 20 hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hii ni kwa sababu kutoa manii mara kwa mara huondoa sumu katika korodani.
Vilevile ufanyaji wa mapenzi mara nyingi hupunguza uwezekano wa kuugua mafua na kuondoa bakteria ndani ya mwili.
Watafiti wa chuo cha Wilkes-Barre nchini Pennsylvania wamegundua kuwa, watu wanaojamiiana mara moja au mbili kwa wiki wanaburudika kwa kiwango cha asilimia 30 na pia huimarisha mfumo wa kinga ya mwili (Immunoglobulin A) ukilinganisha na wale ambao hufanya mara chache au wasiofanya kabisa.
‘Immunoglobulin A (IgA)’ ni mfumo unaoulinda mwili dhidi ya virusi na bakteria wa aina mbalimbali.
Madhara ya kupata UTI hupungua kwa kiwango cha kufikia asilimia 80 ndani ya saa 24 mtu anapojamiiana. Wakati wa kujamiiana bakteria ndani ya uke husukumwa kwenye mirija ya mkojo na hutolewa nje. Hivyo kwa wanawake pale wanapoacha kujamiiana huongeza hatari ya kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Malumbano ndani ya mahusiano huweza kuanzishwa na; Kutokujamiiana kitu ambacho huichukua furaha, ukaribu na maelewano ndani ya mahusiano.
“Kutokujamiiana ndani ya ndoa kunaweza kupunguza kujiamini na kujithamini na pia hupunguza kiwango cha homoni ambayo hutumiwa na mwili kama dawa na pia kuwezesha kujifungua.” Anasema Les Parrott, ambae ni mwanasaikolojia na mwandishi wa kitabu cha “Saving Your Marriage Before it starts”
Kutokujamiiana kwa muda mrefu huongeza woga na kuhisi kuwa mwenza wako anaweza kuchepuka na kutafuta mwingine ambae atamtimizia haja yake ya kujamiiana kitu ambacho kinaweza kuleta mafarakano ndani ya ndoa.
Lengo la Parrott siyo kwamba wachumba wasiojamiiana hawana furaha, la hasha “kujamiiana ni njia mojawapo ya kuelezea ama kuonesha urafiki uliopo kati ya wenza hao”
Busu, kushikana mikono, na kupeana zawadi husaidia pia kuwaunganisha wapenzi kihisia hata kama wasipokutana kimwili.
Vilevile wanaume ambao hawajamiiani mara kwa mara na wasiojamiiana kabisa huongeza uwezekano wa kupata madhara ya uume kushindwa kusimama. Hii ni kulingana na utafiti uliotolewa na American Journal of Medicine.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post