MAHAKAMA KUU DAR YATUPILIA MBALI OMBI LA FREEMAN MBOWE

Mahakama Kuu Dar es Salaam leo imetupilia mbali ombi la Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe la kutaka Jeshi la Polisi kutomkamata na kumtia kizuizini kufuatia kesi ya biashara ya dawa za inayomkabili.
Wiki iliyopita mahakama ilizuia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kutomkamata kiongozi huyo na kumuweka kizuizini hadi hapo pingamizi la serikali litakapotolewa uamuzi na mahakama.
Serikali iliweka pingamizi kufuatia ombi hilo la Freeman Mbowe ambapo walitaka mahakama kutokubali ombi la Polisi kutomkamata Mbowe.
Aidha, kwa kipindi ambacho uamuzi huu haukuwa umetolewa, Jeshi la Polisi halikuwa linaruhusiwa kumkamata Mbowe na kumuweka kizuizini lakini waliruhusiwa na mahakama kumuita kwa ajili ya mahojiano pale wanapoona inafaa.
Mbowe ni miongoni mwa watuhumiwa 65 waliotajwa majina yao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwatuhumu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post