MAKALA: SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA CHANGAMOTO ZAKE

SHARE:

Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, wanawake duniani kote huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini kupitia shughuli mbalimbali za maendel...

Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, wanawake duniani kote huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo walizofanya, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.
Akiongea hivi karibuni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko”
Kauli mbiu hii inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, kibiashara, upatikanaji wa mitaji, masoko na biashara ili waweze kushiriki kwa usawa, na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji.
“Ujumbe wa kauli mbiu hii umezingatia sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000 na ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu hususani lengo namba 5 kuhusu usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi” amesema Nkinga.
Kauli mbiu ya mwaka huu imetotolewa kutokana na kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa (UN) isemayo “Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi katika Dunia ya Mabadiliko ya Kazi”.
Akizungumza hivi karibuni, Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) Edda Sanga alisema kuwa wanawake  wanapaswa kujiwezesha katika maeneo ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii ili wapate fursa ya kushiriki katika maamuzi mbalimbali ambayo hatimaye yatawaletea tija na mafanikio.
Hii ina maana kuwa, endapo wanawake watapata nafasi ya kushiriki katika maamuzi mbalimbali ni rahisi kwao kusikilizwa na hata kuwa na sauti katika masuala ya wao kumiliki ardhi, majumba na hata viwanda.
Aidha, kauli mbiu hii inawahamasisha wanawake kuhakikisha kuwa kunakuwa na usawa wa jinsia unaoondoa vikwazo na kuhakikisha wanapata fursa sawa na kuweka ulinganifu katika ushiriki ambao unawanufaisha kiuchumi kuanzia ngazi ya familia.
Ili kufikia malengo ya kujikomboa kiuchumi, wanawake wanatakiwa kujitambua na pia kutambua malengo na mipango yao. Wanatakiwa kutambua na kutumia fursa vizuri wanayopata hasa mahali watakapopata taarifa za kuwanufaisha kiuchumi kwa mfano benki, vikundi vya mikopo, taasisi au hata kwa watu binafsi.
Kumekuwa na juhudi mbalimbali za kuwakwamua wanawake kiuchumi, kutoka kwenye taasisi, mashirika na watu binafsi,  hata hivyo wao pia wanahitaji kujikomboa kwa kutumia juhudi zao binafsi kama vile kujiunga katika vikundi waweze kukopeshwa ili waweze kujiajiri katika mkondo wa uzalishaji mali, kama vile kuanzisha viwanda vidogo vidogo, kwa mfano viwanda vya usindikaji vyakula, kazi za mikono na ushonaji ambavyo havihitaji mtaji mkubwa.
Hii itawafanya kunufaika na kuondoa hali ya utegemezi katika jamii, na hivyo kujiondoa katika hali ya unyonge.
Ni ndhahiri wanawake ndio wazalishaji wakubwa katika nyanja za kiuchumi, hivyo katika kutimiza ndoto na malengo zao ni budi juhudi zitumike ili washiriki katika kukuza pato lao na taifa kwa ujumla.
Naye Lilian Liundi ambaye ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) anasema kuwa katika kusherekea siku ya wanawake duniani, taasisi yao ilifanya  kongamano  hivi karibuni pamoja na mambo mengine walizungumzia mpango wa taifa kuhusu ushiriki wa wanawake katika kuelekea uchumi wa viwanda vya kati.
Alisema kuwa wanawake wa mjini kwa sasa wanashiriki vizuri katika shughuli ambazo huwaongezea kipato wakati wanawake  wa vijijini ushiriki wao katika shughuli za kuwaongezea kipato si wa kuridhisha kwani wanatumia muda mrefu kutembea kutafuta maji na kuni kwa ajili ya matumizi ya familia.
Liundi ametoa wito kuwa huduma za jamii zisogezwe karibu na jamii ili wanawake ambao ni wazalishaji mali wakubwa wapate muda wa kutosha kushiriki katika shughuli za kujiongezea kipato badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Magreth Dotto ambaye ni Mhandisi wa Migodi, na Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amewashauri watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi kwa kuzingatia kasi ya ukuaji wa teknolojia kila siku ili baadaye wapate nafasi nzuri katika jamii na kutoa mchango wao katika kutatua changamoto za kijamii na taifa.
“Uhandisi unawezekana kwa wasichana na ni taaluma nzuri, hivyo wasichana waache kuyaogopa masomo ya sayansi, ni taaluma inayobadilisha maisha kwa kuyaboresha kwa sababu inalipa vizuri” amesema Magreth.
Kwa upande wake Dkt. Ave Maria Samakafu ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya Wanawake ya Ulingo alisema kwa sasa wanawake wana mwamko mkubwa ambao umeleta mageuzi katika familia na kuinua kipato chao.
“Kwa sasa tunaona ushiriki mkubwa wa wanawake katika nyanja ya uchumi kwa sababu kuna wanawake wafanyabiashara wadogowadogo, wa kati na hata wakubwa” anasema Dkt Semakafu.
Amesema kuwa elimu inahitajika zaidi kwa wanawake wa vijijini ambao bado wanatawaliwa na tafsiri potofu ambapo ukandamizaji wa wanawake bado unapewa nafasi kubwa na jamii, hivyo kuwafanya wasisonge mbele katika kujiletea maendeleo yao.
Dkt. Semakafu aliendelea kusema kuwa wanawake wengi wa mjini wanatambua nafasi zao katika jamii, hivyo wanatumia ufahamu huo kama fursa kwao ambazo zinawasaidia katika kuleta mageuzi ndani ya familia zao.
“Vijana wa kike wamekuja na nguvu mpya, kinachoendelea sasa hivi kinafungua uelewa wa jamii, watoto na wazazi na kuwafanya watambuliwe na jamii” alisema Dkt. Semakafu.
Dkt. Semakafu ametoa mfano unaodhihirisha nafasi ya mwanamke akimtaja Agnes Magongo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya UN ya “women economic empowerment” ambayo ni tuzo ya uwezeshaji wa wanawake.
“Wanawake tushiriki katika kuboresha maisha yetu, tusiwe wasindikizaji bali watendaji, twende pamoja katika uchumi wa viwanda ili tuweze kumiliki viwanda” alimalizia Dkt. Semakafu.
Katika kuhimiza fursa za uchumi kwa wanawake kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote nchini kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake ili waweze kushiriki na kunufaika nazo hasa kipindi hiki ambapo Tanzania inaelekea azma ya uchumi wa kati kwa misingi ya kuwa nchi ya viwanda.
Mama Sihaba aliwakumbusha wadau wote katika ngazi zote kuweka mikakati thabiti ya kutatua changamoto zinazokwamisha kufikiwa kwa usawa wa jinsia na kusababisha wanawake na wasichana kushindwa kutimiza malengo na ndoto zao kimaisha.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKALA: SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA CHANGAMOTO ZAKE
MAKALA: SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA CHANGAMOTO ZAKE
https://1.bp.blogspot.com/-mar8KH3Guro/WL-LTgrnvXI/AAAAAAAAXm4/gOJu0gkhA6YhOJV2gjkX6B4qt6oPidTFwCLcB/s1600/kike.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mar8KH3Guro/WL-LTgrnvXI/AAAAAAAAXm4/gOJu0gkhA6YhOJV2gjkX6B4qt6oPidTFwCLcB/s72-c/kike.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/makala-siku-ya-wanawake-duniani-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/makala-siku-ya-wanawake-duniani-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy