MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA MKOA WA DODOMA

SHARE:

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitend...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 14-Mar-2017 wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya Kikosi Kazi kilichoundwa na serikali kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za Serikali kuhamia Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kujiimarisha na kujipanga ipasavyo katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo hasa wakati huu ambao serikali inahamia Dodoma.
Ameonya kuwa wawekezaji matapeli kamwe wasipewe nafasi ya kuwekeza Dodoma na ametaka uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwa makini makundi hayo ili wasije kuvuruga mipango ya serikali ya kujenga Makao makuu ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma.
Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.
Amesema amefurahishwa na kasi ya uongozi wa mkoa wa Dodoma jinsi unavyojipanga katika kuhakikisha azma ya serikali ya kuhamia Dodoma inafanikiwa kwa haraka ikiwemo utengaji wa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na huduma za kijamii.
Kuhusu maeneo ya wafanyabiashara wadogo, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Dodoma wahakikishe wanatenga haraka maeneo maaluma kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ili nao waweza kunufaika na mpango wa Serikali kuhamia mkoani Dodoma.
“Ni muhimu maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili wafanyabiashara wadogo  yawe huduma zote za msingi ili kusaidia wafanyabiashara hao waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi “Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwashirikisha viongozi wa wafanyabishara wadogo kuhusu maeneo yatakayotengwa ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabishara hao kupewa maeneo yasiyofaa wa ajili ya shughuli zao.
Awali kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kuzungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alimweleza Makamu wa Rais mipango na mikakati ya mkoa huo kuhusu azma ya serikali ya kuhamia Dodoma ikiwemo uimarisha wa huduma za msingi ikiwemo afya, miundombinu, maji na elimu.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amesema mpaka sasa kazi ya kuainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji, makazi na mahali ambapo ofisi za serikali na za mabalozi zitajengwa umeshakamilika.
Amesema uongozi wa mkoa wa Dodoma utaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali, mashirika ya kimataifa na mabalozi ili kuhakikisha maeneo  yaliyotengwa yanaendelezwa haraka.
Ameeleza kuwa ujenzi wa miji Mitano mikubwa mkoani Dodoma na ujio wa wawekezaji mbalimbali utaufanya mkoa huo kuwa na uhitaji nishati ya umeme ya uhakika hivyo amehimiza ujenzi wa bomba la gesi asili kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ukafanyika haraka.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dodoma
14-Mar-2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA MKOA WA DODOMA
MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA MKOA WA DODOMA
https://1.bp.blogspot.com/-NN0fbmZPPW8/WMg8dHDsMuI/AAAAAAAAX54/nO6_CIweVn0EJY-MqogUnwSTP8T0HC16QCLcB/s1600/makamu-wa-rais-750x375.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-NN0fbmZPPW8/WMg8dHDsMuI/AAAAAAAAX54/nO6_CIweVn0EJY-MqogUnwSTP8T0HC16QCLcB/s72-c/makamu-wa-rais-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/makamu-wa-rais-atoa-maagizo-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/makamu-wa-rais-atoa-maagizo-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy