MALKIA WA UINGEREZA AJIBU BARUA YA MTOTO


                     

Mtoto wa miaka sita anayependa kuvaa kama walinzi wa Malkia, amepokea kwa furaha majibu ya barua yake aliyokuwa amemwandikia Malkia wa Uingereza.
George Mearing, anayeishi Basingstoke, Hampshire, aliandika barua na kuituma kwa Malkia akieleza ni kwa namna gani anapenda kuvalia kama wanajeshi na angependa kuwa miongoni mwa kundi la walinzi wa kifalme wanaomlinda Malkia.
Aliambatanisha picha zake akiwa amevalia sare za kitamaduni za rangi ya Nyekundu na Nyeusi.
Katika barua yake aliyoiandika kwa mkono alisema “Nimekuwa nikijifunza kukuhusu wewe, familia yako na wanajeshi wanaokulinda. Mimi na mama yangu tumewahi kutembelea ngome ya Windsor mara kadhaa. Ninapenda kuvalia kama mwanajeshi. Nitafurahi sana kama nitapata barua kutoka kwako.”
The note George sent to the Queen said how he likes dressing up as soldiers
Kijana George alivutiwa sana na familia ya kifalme pale alipoona askari wakiwa wamevalia sare nyekundu wakati wa maadhimisho ya miaka 90 ya kuzaliwa kwa Malkia hapo mwaka jana.
Helen, mama wa George alisema “niliona bahasha  na mara moja nikajua ilikotoka. Sikuifungua bali niliiacha ili mwanangu aje aifungue mwenyewe. Alipoiona alifurahi sana na uso wake ulijawa na tabasamu kwa kupokea barua kutoka familia ya kifalme anayoipenda.”
The youngster received a letter from the Queen's Lady-in-Waiting with the royal seal
Malkia aliomba samahani kwa George kwa kushindwa kuijibu barua ile yeye mwenyewe, lakini alifurahishwa kusikia kuwa George amefurahia kujifunza kuhusu familia ya kifalme na walinzi wa malkia.
The letter also contained leaflets and information of the guards and their manoeuvres - including the changing of the guard                          George is a huge fan of the Royal Family and has visited Windsor Castle several times
                 George pictured standing next to a Queen's Guard

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post