MAMA SAMIA MGENI RASMI UKARIBISHO WA VIONGOZI DODOMA

Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma mahali ambapo kutafanyika sherehe za kuwapokea viongozi mbalimbali wa serikali baada ya kuhamia Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla maalumu ya kuwakaribisha viongozi wa Serikali itakayofanyika Machi 5 mwaka huu mkoani Dodoma.
Hafla hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma na itafanyika mkoani humo katika viwanja vya Nyerere (Nyerere Square) kuanzia saa 8 kamili mchana.
Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Jeremia Mwakyoma ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ujio wa viongozi hao katika Mkoa huo.
Mwakyoma amesema viongozi wa Serikali kuhamia katika Makao Makuu ya Nchi ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo Mkoa utawakaribisha rasmi Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara waliohamia kutoka Jijini Dar es Salaam.
“Tukio la viongozi wa Wizara kuhamia Makao Makuu Dodoma ni la kihistoria ndio maana uongozi wa Serikali ya Mkoa umeona ni vema kuweka utaratibu rasmi wa kuwakaribisha viongozi hao,”alisema Mwakyoma.
Afisa Habari Mwakyoma amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa huo pamoja na Mikoa ya jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye hafla hiyo.
Mnamo Julai 25 mwaka 2016 katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yalioadhimishwa mkoani Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli alitangaza rasmi Serikali kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Nchi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post