MAMBO MATANO MAKUBWA YATAKAYOTIKISA NCHI NZIMA MWEZI HUU

SHARE:

Dar es Salaam. Mwezi wa tatu maarufu kama Machi ulioanza leo, umegubikwa na matukio matano ambayo Watanzania kutoka pande zote za n...Dar es Salaam. Mwezi wa tatu maarufu kama Machi ulioanza leo, umegubikwa na matukio matano ambayo Watanzania kutoka pande zote za nchi wanatarajiwa kuyashuhudia.
Tayari Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kilishazungumza takriban mwezi mzima uliopita juu ya kusudio la kutangaza mgogoro na Serikali unaolenga kudai haki ya madai ya wanachama wake.
CWT imekuwa ikilalamika kwa muda sasa juu ya madai mbalimbali ya walimu, yakiwamo yanayohusiana na mishahara na malipo mengine.
Rais wa chama hicho, Gratian Mkoba anasema madai ya walimu yanafikia takriban Sh800 bilioni na awali waliitaka Serikali iwe imeyalipa ifikapo Februari 28, vinginevyo wataanza mgogoro huo leo.
Katika kukoleza chumvi kwenye kidonda, Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema jana kwamba, wanaunga mkono hatua zozote zitakazochukuliwa na CWT kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuwalipa madai yao.
“Tunawanga mkono CWT waendelee na mchakato wao kwa sababu Serikali haitaki kutoa kauli zenye kuwaletea matumaini walimu,” alisema.
Mbali ya sakata hilo, suala lingine linalokusudiwa kuutikisa mwezi huu nchini ni mfumo wa kubadili mtandao wa simu bila ya kubadili kadi (MNP).
Mfumo huo unawapa uhuru wateja wa mitandao yote ya simu nchini kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine wakati wowote wanaoona unafaa.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa atazindua rasmi mfumo huo leo katika ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema lengo ni kuwapa uhuru wateja kutumia mtandao bora zaidi na kuongeza ushindani kwa kampuni ili kuboresha huduma zao.
“Uanzishwaji wa MNP ni kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2011. Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwezesha huduma hii katika mitandao yao,” alisema Kilaba.
Mbali na mambo hayo mawili, lingine la tatu ni lile la waumini wa madhehebu ya Kikristo nchini na duniani kote kuanza mwezi wa kujinyima kukumbuka mateso ya Yesu Kristo kwa kufunga kula, maarufu kama kipindi cha Kwaresma.
Wakristo duniani kote kuanzi leo watasali katika Jumatano ya Majivu, misa ambayo ni ufunguzi rasmi wa kipindi cha Kwaresma.
Ibada ya Majivu huhusisha waumini kupaka majivu ikiwa ni ishara ya mwanzo wa kuanza mfungo wa siku 40 wa kukumbuka mateso ya Yesu Kristo.
Jambo lingine ni lile la marufuku ya viroba ambalo zuio lake linaaza leo.
Iwapo utekelezaji wake utakuwa na ufanisi utasaidia kuzuiliwa kwa pombe hizo kali zinazowekwa kwenye pakiti za plastiki, maarufu kama viroba.
Utekelezwa wa marufuku hiyo ya Serikali unaanza huku kukiwa na uwezekano wa wadau wa biashara hiyo kufungua kesi kupinga utekelezwa wa agizo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Sakata hilo lilianza Februari 20 wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, January Makamba alipotangaza marufuku hiyo huku akiwataka watengenzaji wa pombe hizo watafute utaratibu ulioandaliwa na Serikali wa kutumia chupa badala ya mifuko midogo ya plastiki.
January aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, operesheni ya kukagua utengenezaji, uuzaji na matumizi  ya pombe ya viroba itaendeshwa na kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira za ngazi zote kuanzia mkoa hadi mtaa ambazo zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni hiyo Tamisemi.
“Ukikutwa unakunywa, unauza na utengeneza au kuingiza viroba utachukuliwa hatua kali zikiwamo faini na kifungo au vyote kwenda sambamba,” alisema waziri huyo.
Mwezi huu pia unaanza huku awamu ya kwanza ya taasisi za Serikali kuhamia na kuanza rasmi shughuli zake mjini Dodoma baada ya kazi ya uhamaji kumalizika jana.
Agizo la kuhamia Dodoma lilitolewa na Rais John Magufuli mwaka jana kuwa, kabla ya kumaliza miaka mitano ya awamu ya kwanza ya utawala wake, Serikali itakuwa imehamia Dodoma.
Baada ya tangazo hilo la Rais Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitikia wito huo wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa mjini Dodoma, akitaka nyumba yake ikamilike haraka.
Pia alitangaza kuwa awamu ya kwanza ya uhamaji itahusisha mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao na wasaidizi wao, huku ile ya pili itaanza Julai baada ya Bunge la Bajeti. Uhamaji huo utakuwa kwa awamu sita na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 pale
Rais atapohamia rasmi mjini humo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAMBO MATANO MAKUBWA YATAKAYOTIKISA NCHI NZIMA MWEZI HUU
MAMBO MATANO MAKUBWA YATAKAYOTIKISA NCHI NZIMA MWEZI HUU
https://3.bp.blogspot.com/-A78xSshiTDc/WLaYMlbb2oI/AAAAAAAAXDI/AKAGJxz2klUm8qQ4IeZ6ziPaGmROzY0UwCLcB/s1600/MATANO.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-A78xSshiTDc/WLaYMlbb2oI/AAAAAAAAXDI/AKAGJxz2klUm8qQ4IeZ6ziPaGmROzY0UwCLcB/s72-c/MATANO.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/mambo-matano-makubwa-yatakayotikisa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/mambo-matano-makubwa-yatakayotikisa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy