MARCO VERRATTI KUBAKI PARC DES PRINCES

Wakala wa kiungo kutoka nchini Italia Marco Verratti, amemaliza uvumi wa mchezaji wake kuwa mbioni kuihama klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo huyo alitajwa kuwa kwenye harakati za kutaka kujiunga na klabu bingwa nchini Italia Juventus ama FC Barcelona ya Hispania.
“Marco atabaki PSG,” alisema wakala Donato Di Campli alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa ligi ya Italia kati ya Atalanta, ambao walishinda mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Pescara mjini Bergamo.
“Ana mkataba hadi mwaka 2021, hivyo ataendelea kubaki Ufaransa. Kwa sasa ninaweza kuwaeleza hivyo, kwa sababu tunaheshimu mkataba wake.
“Endapo watatuambia wanataka kumuuza mwishoni mwa msimu huu, tutafanya mipango ya kuhakikisha anapata klabu itakayomfaa.”
Verratti hajawahi kucheza katika ligi ya Serie A, tangu alipoisaidia klabu ya Pescara kupanda daraja ikitokea Serie B mwaka 2012.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post