MASAUNI ATOA WIKI MOJA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUANZISHA KITUO WILAYANI RUANGWA

SHARE:

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni( katikati ) Na Felix Mwagara/MOHA  NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi...

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni( katikati )
Na Felix Mwagara/MOHA 

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha kituo cha zimamoto Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.   

Masauni alisema Aprili Mosi mwaka huu Jeshi hilo litakuwa na ofisi wilayani humo ili askari wa Jeshi hilo waanze kutoa huduma sehemu mbalimbali ya Wilaya hiyo ambayo ni muhimu kituo hicho kuwepo kutokana na uwepo na machimbo ya madini ya dhahabu pamoja na mji kuendelea kukua kwa kasi.  

“Tumekubaliana vizuri baada ya Kamanda wa Zimamoto mkoa kuwa ifikapo tarehe moja askari wa zimamoto watakuwepo hapa Ruangwa rasmi kwa ajili ya kuanza kazi, na watapewa ofisi na halmashauri ya Wilaya, hivyo utaratibu wa kupata vifaa vya awali uanze mara moja kama tulivyokubaliana,” alisema Masauni. 

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Lindi, Christina Sunga alimuhakikishia Naibu Waziri pamoja na Watendaji wa Wilaya hiyo, agizo hilo atalifanyia kazi haraka iwezekanavyo na mpaka ifikapo Aprili mosi mwaka huu tayari askari wawili watakuwa wameripoti mjini Ruangwa.  

“Uwepo wa askari hawa kutarahisisha kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuzima moto pamoja na kupambana na uzimaji moto, licha ya kuwa tunakuwa na vifaa vya awali vya uzimaji moto mpaka hapo tutakapopata gari kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzimaji moto na utoaji elimu zaidi,” alisema Sunga na kuongeza;  

“Tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kutupa ofisi kwa ajili ya askari wa zimamoto lakini pia kutuwezesha kupata vifaa hivyo vya awali vya uzimaji wa moto.” 

Aidha, Masauni alimuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, (RPC) Renatha Mzinga kuandaa mchoro pamoja na gharama ya ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa ili ujenzi huo uanze.  

“Nimekagua eneo la ujenzi wa kituo kipya cha polisi, eneo zuri na linafaa kwa ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi, maandalizi tayari yameanza na hivi karibuni RPC atakamilisha mchoro pamoja na gharama ya ujenzi wa kituo hicho hapa Ruangwa,” alisema Masauni.  

Pia Masauni amesema Wizara yake itahakikisha inawajengea ofisi Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani humo ambapo kwasasa ofisi hizo zipo katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo. 

Naibu WaziriMasauni amemaliza ziara yake ya siku mbili kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na askari na maafisa wa vyombo walio chini ya wizara yake mkoani Lindi na tayari amesafiri mkoani Mtwara kuendelea na ziara yake.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MASAUNI ATOA WIKI MOJA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUANZISHA KITUO WILAYANI RUANGWA
MASAUNI ATOA WIKI MOJA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUANZISHA KITUO WILAYANI RUANGWA
https://1.bp.blogspot.com/-kJ-PvZ73c5Y/WNTKZSiosmI/AAAAAAAAYmg/gSprVsluvjUGzRRD62rpOdcNoAbxFwE6ACLcB/s1600/PIX%2B1%25281%2529.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-kJ-PvZ73c5Y/WNTKZSiosmI/AAAAAAAAYmg/gSprVsluvjUGzRRD62rpOdcNoAbxFwE6ACLcB/s72-c/PIX%2B1%25281%2529.JPG
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/masauni-atoa-wiki-moja-kwa-jeshi-la.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/masauni-atoa-wiki-moja-kwa-jeshi-la.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy