MASHABIKI 200 WA ARSENAL WAANDAMANA KUTAKA KOCHA WENGER AJIUZULU

Mashabiki wapatao 200 wa timu ya Arsenal wameandamana na mabango jana usiku katika uwanja wa Emirates kushinikiza kocha wao Arsene Wenger ajiuzulu.

Wanachama hao wa Arsenal wanataka uongozi wa klabu hiyo kutomuongezea kocha Wenger mkataba mpya huku wakisema anaiuwa klabu hiyo.

Usiku wa jana ulijidhihirisha kuwa ni janga kwa Arsenal na kwa kocha Wenger baada ya kufungwa magoli 5-1 na timu ya Bayern Munich.
Mashabiki wa Arsenal wakiandamana na bango lililoandikwa "Kila hadithi nzuri inamwisho wake" ikiwa ni ujumbe kwa kocha Wenger


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post