MAUAJI YA VIONGOZI KIBITI YAZUA TAHARUKI

Kibiti. Mfululizo wa mauaji yanayotokea katika wilaya ya Kibiti, umezua taharuki baada ya jumla ya viongozi wanane wa serikali  kuuawa katika  kipindi miezi kumi.

Katika tukio la hivi karibuni, ambalo Ofisa wa upelelezi wa polisi, Peter Kubezwa aliuawa,  wauaji waliacha orodha ya   viongozi wa  vijiji wanaowasaka ili wawaue.

Kadhalika, katika tukio hilo la mauaji ya Kubezwa, Ofisa ukaguzi wa Maliasili Peter Kitundu na mlinzi, Athuman Ngambo pia waliuawa.   Wauaji hao hawakuchukua kitu chochote baada ya mauaji hayo.

Wengine waliouawa wilayani humo katika kipindi hicho ni pamoja na  Mwenyekiti  wa kijiji  cha Nyambunda, Saidi Mbwana, aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho,  Ally Milandu na  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamili, Ally Saleh.

Wengine waliouawa ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyang’undu, Mohamed Thabiti aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mjumbe wa serikai ya kijiji cha Nyambunda, Oswald Mrope.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post