MAWAZIRI WANNE AMBAO MATAMKO YAO YAMEPINGWA NA RAIS DKT MAGUFULI

SHARE:

Jana mjadala mzito umeibuka kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Rais Dkt Magufuli kufuta kauli ya Waziri wa Katiba n...

Jana mjadala mzito umeibuka kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Rais Dkt Magufuli kufuta kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe iliyokuwa ikitaka wananchi wote kuwa na vyeti vya kuzaliwa kabla ya kufunga ndoa.
Waziri Mwakyembe akitoa tamko hilo alisema kuwa, hakuna ndoa yeoyote itakayofungwa iwe ya kimila, kiserikali au kidini ambayo wahusika wake watakuwa hawana vyeti vya kuzaliwa.
Akieleza dhumuni la uamuzi huo, Waziri Mwakyembe alisema serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.
Jana asubuhi kabla ya kuaza safari ya kurejea Dar es Salaam kutoka Dodoma, Rais Dkt Magufuli ilifuta uamuzi huo huku akisema ungezuia watanzania wengi kuoana kwani watanzania wenye vyeti hivyo ni chini ya asilimia 20.
“Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji” alisema Rais Dkt Magufuli
“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Lakini si Waziri Mwakyembe pekee ambaye agizo lake limewahi kutenguliwa na Rais Dkt Magufuli. Wamo mawaziri wengine watatu ambao walitoa matamko lakini yakabatilishwa na Rais Dkt Magufuli.
Wa kwanza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ambapo Machi 3, 2016 alitangaza kumteua Dkt. Carina Wangwe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Lakini muda mfupi baadae waziri huyo alibatilisha agizo hilo.
Baada ya Waziri Mhagama kubatilisha uteuzi huo, Rais Dkt Magufuli alimteua aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Godius Kahyarara kushika nafasi hiyo.
Mwingine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene ambaye agizo lake la kuondolewa wafanyabiashara wadogo maeneo ya mijini lilipingwa.
Agosti 12, 2016 Waziri Simbachawene alitangaza kuwa wamachinga wote maeneo ya mijini waondoke mara moja na pia wasitishe kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara na kwamba wapelekwe katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Rais Dkt Magufuli akihutubia katika mkutano wa hadhara jijini Mwanza alitengua uamuzi huo na kusema kuwa machinga wasiondolewe kwenye maeneo wanayofanyia biashara zao. Aidha, Rais Magufuli alisema wanaweza hata kuamua kufunga barabara moja machinga wakafanya shughuli zao hadi hapo watakapopatiwa maeneo mazuri ya kufanyia biashara na si kupelekwa sehemu ambazo hazina wateja.
Waziri wa tatu aliyekumbana na kauli yake kupingwa na Rais Magufuli ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alisema kuwa ‘brand’ za wasanii zilindwe katika vita dhidi ya dawa za kulevya inayoendelea nchini.
Waziri Nape aliyasema hayo alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu wasanii na watangazaji waliotajwa katika orodha ya watumiaji, wasambazaji wa dawa za kulevya na hivyo kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kwa ajili ya mahojiano. Ni rahisi sana kuharibu ‘brand’ ya mtu kwa muda mfupi lakini itakuchukua miaka kuweza kuijenga. Hivyo nasisitiza hekima itumike katika vita hii, alisema Waziri Nape.
Akizungumza katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dkt Magufuli alitupilia mbali hoja hiyo ya kulinda majina ya wasanii aliposema kuwa kwenye vita ya dawa za kulevya asiangaliwe mtu ni nani, ukubwa wa jina lake au cheo chake kwenye jamii, kila anayehusika achukuliwe hatua.
Kuonyesha msisitizo, Rais Dkt Magufuli alisema kuwa hata mke wake kama anatuhumiwa kuhusika na biashara hiyo, akamatwe kwa sababu madhara ya dawa hizo ni makubwa katika jamii yetu.
Watu mbalimbali waliotoa maoni yao kuhusu uamuzi wa Rais Dkt Magufuli wa jana, waliilaumu serikali kwa kukosa mawasiliano na ushirikiano. Aidha walieleza kuwa baadhi ya viongozi wataogopa kutoa maagizo kutokana na hofu kuwa huenda yakapingwa na kiongozi wa nchi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAWAZIRI WANNE AMBAO MATAMKO YAO YAMEPINGWA NA RAIS DKT MAGUFULI
MAWAZIRI WANNE AMBAO MATAMKO YAO YAMEPINGWA NA RAIS DKT MAGUFULI
https://3.bp.blogspot.com/-S_wIYiXyTmI/WMzz1SPMPCI/AAAAAAAAYHI/CvB0RjAzegIrlkTjiZr2aCdFq658YWkhACLcB/s1600/Mwakyembe-akiteta-jambo-na-Rais-John-Magufuli.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-S_wIYiXyTmI/WMzz1SPMPCI/AAAAAAAAYHI/CvB0RjAzegIrlkTjiZr2aCdFq658YWkhACLcB/s72-c/Mwakyembe-akiteta-jambo-na-Rais-John-Magufuli.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/mawaziri-wanne-ambao-matamko-yao.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/mawaziri-wanne-ambao-matamko-yao.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy