MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga  Jumatatu Machi 13, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaounda kikosi hicho.

Taifa Stars, inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/826-mayanga-atangaza-kikosi-cha-taifa-stars

MALINZI AWAPA MAAGIZO MAZITO MAKOCHA WAPYA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amewazawadia makocha wapya 27 waliofuzu kozi ya ukocha kwamba kila mmoja mmoja atampa koni 20 na vizibao 22 kwa ajili ya mazoezi.

Rais Malinzi alitoa ahadi hiyo wakati wa hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’ kwa makocha waliohitimu. Rais Malinzi alialikwa na waratibu kuwa mgeni rasmi ambaye awali, alishangazwa kwa namna ilivyoratibiwa kwa kufuata miongozo ya TFF na CAF.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


 http://tff.or.tz/news/825-malinzi-awapa-maagizo-mazito-makocha-wapya

MALINZI AMLILIA SIR GEORGE KAHAMA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu Sir George Kahama aliyefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais Malinzi amesema taifa limepoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania maendeleo ya mpira wa miguu baada ya kupigania Uhuru ambao Watanzania leo wanajivunia amani.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

malinzi-amlilia-sir-george-kahama

SERENGETI BOYS WAANZA KAMBI

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys imeanza mazoezi rasmi leo Machi 12, 2017 kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Serengeti Boys itakuwa kambini Dar es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/823-serengeti-boys-waanza-kambi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post