MBAPPE ATAKA AACHWE AVUTE PUMZI, AMEZEWA MATE NA WABABE

Mshambuliaji kinda anayetikisa barani Ulaya kwa uwezo wake wa kupachika mabao, Kylian Mbappe amesema anahitaji muda zaidi kujifunza kabla hajatua katika klabu kubwa zaidi.
Mbappe ambaye amefanya vizuri katika msimu wake wa pili akiwa na Monaco, akitingisha nyavu mara 19 katika michezo 32, ametajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaomezewa mate na klabu zote kubwa za Ulaya.
Mbali na Real Madrid na Chelsea, Kocha Jose Mourinho anadaiwa kuapa kumnasa kinda huyo na kwamba atamgeuza kuwa Messi and Cristiano Ronaldo akiwa Old Trafford.
Hata hivyo, kinda huyo mawataka wadau wa michezo kumuacha avute pumzi kidogo kabla hajafanya maamuzi huku akisisitiza kuwa bado anaitumikia Monaco.
“Real Madrid? kwa sasa nipo Monaco ila tutaona kitakachotokea. Madrid ni klabu kubwa sana ila nina mengi ya kujifunza, ni timu ambayo unaenda ukiwa umekuwa vizuri na kiwango chako kipo juu zaidi,” alisema Mbappe.
Mbappe amehusishwa zaidi na klabu ya Madrid hivi karibuni huku beki na nahodha wa klabu hiyo Sergio Ramos akisema watamkaribisha kwa mikono miwili klabuni hapo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post