MBARAWA AWATAKA WADAU KUCHUNGUZA VYANZO VYA AJARI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa usalama wa barabarani nchini kushirikiana na kufuatilia kwa makini vyanzo ajali na kuunganisha nguvu kazi ili kupunguza matukio hayo yanayosababisha vifo na ulemavu kwa watu wengi. 

Profesa Mbarawa aliyasema hayo leo kwenye mafunzo ya mbinu za haraka za kufuatilia ajali, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la barabara(IRF).

 Shirikisho hilo linakutanisha wadau 196 kutoka mataifa manane.

“Ni muhimu kuunganisha nguvu ili kuimarisha utekelezaji wa sheria, ili kupunguza vifo vya watu kwenye ajali za barabarani ni jambo linalohumiza kusikia basi limepata ajali abiria wote wamekufa, tutakuja kuulizwa kutokana na nafasi zetu tulizo nazo mimi kama waziri husika, Sumatra au mkuu wa kikosi cha usala wa barabarani,” alisema.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mafunzo hayo nchini, Joseph Haule alisema tatizo la ajali za barabarani barani Afrika linapaswa kutatuliwa kwa mbinu shirikishi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post