MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AHOJIWA KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Kasi ya mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya imezidi kushika kasi ambapo Mbunge wa Chalinze Mkoa wa Pwani, Ridhiwani Kikwete amehojiwa kwa muda wa saa tatu na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa katika gazeti la JAMHURI, Ridhiwani Kikwete alitajwa katika orodha ya majina 97 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyakabidhi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
Mtoa habari wa gazeti hilo ameeleza kuwa walipoliona jina la Ridhiwani katika orodha hiyo walijua hapa serikali inafanya maigizo kwa sababu hawataweza kumuhoji, kwa madai kuwa yeye ni mtu mzito.
Hakika serikali imebadilika, hakuna atakayepona. Baada ya Ridhiwani kuhojiwa tunaamini sasa hata hao maaskari na mahakimu waliotajwa muda si mrefu nao watatiwa mbaroni, alisema mtoa habari huyo.
Kiongozi huyo alihojiwa Jumatatu Machi 6, 2017 ambapo alifika katika ofisi hiyo majira ya 5:09 asubuhi akiwa amefuatana na watu wengine watatu.
Ridhiwani Kikwete baada ya kufika ofisini hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu cha mahojiano ambapo alihojiwa kwa saa tatu ambapo inaelezwa kuwa alibainika kuwa si muuzaji wala mtumiaji wa dawa hizo, lakini tatizo ni rafiki zake ambao yupo karibu nao.
Wahenga husema kuwa, Ukikaa karibu na uaridi, na wewe utanukia. Mamlaka hiyo imempa onyo baada ya kuona rafiki zake wengi wana tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Kufuati hatu hiyo hatofikishwa mahakamani.
Kamishna Mkuu alipoulizwa kuhusu kuhojiwa kwa Ridhiwani alisema kuwa, yeyote yule anayetuhumiwa hatoachwa, atahojiwa na akipatikana na hatia atafikishwa katika vyombo vya sheria hivyo hakuna cha jina kubwa wala cheo kikubwa.
Ni kweli tumemhoji Ridhiwani Kikwete, na mimi naamini ni bora niwachukize baadhi ya watu nifanye kitu ninachoamini kuwa ni sahihi kuliko kufurahisha watu kwa kufanya kitu ambacho si sahihi, alisema Kamishna Sianga.
Ridhiwani Kikwete alipoulizwa alisema kuwa ni kweli amehojiwa na anafuraha kwa kuwa wamebaini hauzi, wala hatumii dawa za kulevya hivyo taharuki iliyokuwepo itakwisha sana.
“Roho yangu imesuuzika na taharuki iliyokuwapo miongoni mwa jamii kwamba huenda nauza dawa za kulevya sasa imeondoka,” alisema Ridhiwani Kikwete.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post