MBUNGE WA CHADEMA AITAKA SERIKALI IHALALISHE BANGI

Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, Esther Matiko ameitaka serikali kufanya utafiti kuhusu madhara ya bangi na kama wataoana madhara ni madogo na faida yake ni kubwa basi waruhusu kuwa  zao la biashara.
Matiko ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha runinga ambapo amekanusha tuhuma za kuhamasisha wakazi wa jimbo lake kulima bangi.
Akieleza sababu za wakazi wa jimbo lake kulima bangi kwa wingi, alisema ni kutokana na serikali kutotoa pembejeo za kilimo lakini pia elimu kuhusu kilimo mbadala cha kuweza kuwaongezea kipato.
Wilaya ya Tarime mkoani Mara ndiyo inayoongoza kwa kulima bangi mkoani mara, kilimo ambacho kimepigwa marufuku nchini kutokana na zao hilo kutajwa miongoni mwa dawa za kulevya.
Matiko si mbunge wa kwanza kuzungumzia suala la serikali kufanyia utafiti kuhusu zao la bangi ambapo awali Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma alisema kuwa bangi inawasaidia watumiaji kufanya kazi, hivyo kama haina madhara waihalalishe.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post