MCHUNGAJI ASHINDA MOCHUARI AKISUBIRI MKE WAKE AFUFUKE

Mchungaji Githumba kutoka Embu nchini Kenya jana alishinda katika chumba cha kuhifadhia maiti nchini humo akisubiria mke wake, marehemu Polly Kagembo afufuke.
Mchungaji huyo alisema kuwa mke wake aliyefariki Jumapili Machi 26, 2017 angefufuka siku ya tatu kama ilivyokuwa ha Lazaro aliyefufuliwa na Yesu.
Baada ya kufunga na kuomba kwa muda tangu saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni katika chumba hicho, siku ya jana ambapo aliamini mkewe angefufuka iliisha bila mafanikio. Mchungaji huyo alikuwa amewataka waandishi wa habari kwenda eneo hilo kujiona muujiza wa mkewe akifufuka.
C8FlCfxWkAE8Kum
Baba huyo mwenye watoto wanne alikuwa akisema mkewe huyo aliyefariki kutokana na kuugua Kifua Kikuu alikuwa amelala tu na angefufuka siku ya tatu kama wangekuwa wakiomba na kumuamini Mungu kwa pamoja.
Mitandao ya kijamii jana nchini Kenya walizungumzia suala hilo ambapo wengi walichapisha habari za kuchekesha kuhusu mchungaji huyo. Kupitia mtandao wa Twitter, wengi waliandika maoni yao kupitia hashtag #PastorGithumba
 what's wrong with people nowadays you thinks that woman would want to resurect na hii mashida iko huku


 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post