MEYA WA UBUNGO KUFUNGUA KESI YA JINAI DHIDI YA RC MAKONDA

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti vya kidato cha nne alivyovitumia si vya kwake.
Jacob ameeleza kuwa kesi hiyo itasimamiwa na mawakili maarufu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Peter Kibatala.
Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 18 mwaka huu ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais.
Mbali na kufungua mashtaka mahakamani, Meya huyo wa CHADEMA amesema kuwa, atamshtaki Makonda katika Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post