MFAHAMU MWANAMITINDO ANAYEUGUA ‘UGONJWA WA PAKA’

SHARE:

Mwanamitindo wa Uingereza, Caitin Stickels mwenye umri wa miaka 29,  amekuwa akisumbuliwa na  tatizo ambalo ni nadra sana la kiafya linal...

Mwanamitindo wa Uingereza, Caitin Stickels mwenye umri wa miaka 29,  amekuwa akisumbuliwa na  tatizo ambalo ni nadra sana la kiafya linalofahamika kama ‘Ugonjwa wa macho ya paka’ unaojulikana kitaalamu kama ‘Schmid-Fraccaro Syndrome.’ ambao humsababishia maumivu makali sana.
Tatizo hilo la kiafya humfanya aonekane kama paka.
Hali yake ilimvutia mpiga picha za mitindo kutoka Uingereza Nick Knight. Alimuona  mwanamitindo huyo kutoka Seattle mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Tangu wakati huo, amevuma kama mwanamitindo na hata picha zake zikachapishwa katika jarida la V Magazine.


Hata hivyo mwanamitindo huyo bado anafurahishwa na mafanikio aliyoyapata licha ya kusumbuliwa na ugonjwa huo.
“Ni mabadiliko makubwa zaidi mema yaliyowahi kutokea katika maisha yangu,” alisema.
Watu wanaougua ugonjwa huo wanaweza kuwa na matatizo katika maumbile ya masikio yao, moyo na kwenye figo. Wakati mwingine, viungo vingine mwilini huathiriwa.
Sura ya Caitin si kama ya wanamitindo wengi ambao wamevuma sana. ‘Urembo’ wake si kama ule ambao wengi wamezoea kuuona ukiangaziwa kwenye majarida, filamu na runinga.
Caitin Stickels
Alisema “Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo au kufikiria ningeshiriki katika tasnia ya mitindo na mavazi,”
Aliongeza kuwa huwa anakumbana na changamoto kadhaa katika maisha yake kutokana na ugonjwa huo unaomsumbua.
“Mafadhaiko kutokana na ugonjwa huu huwa ni ndani ya moyo wangu, lakini kazi yangu ya uanamitindo, uigizaji na uimbaji hunisaidia sana kusahau maumivu niliyo nayo moyoni.” anasema.
Caitin anasema pia hupata maumivu makali mwilini na kupata kichefuchefu.
“Ni figo moja pekee inayofanya kazi, kwa hivyo huwa inanibidi kunywa maji sana. Pia mwili wangu huathiriwa sana na mabadiliko katika mazingira, lakini kwa sababu umekuwa hivyo kwa muda mrefu, watu wengi niliotangamana nao huwa hawatambui kama nina tatizo. Mimi ni mgumu kama jiwe.”
“Nafikiri jambo jingine ni kwamba macho hukaa kama ya paka wakati wote na kusababisha watu kuniogopa. Hii hata hivyo huniwezesha kuona vyema usiku. Nalipenda jua na mara nyingi hutoka nje na kutembea, lakini huwa linaniumiza macho yangu.”
Vile vile aliongeza kuwa pamoja na hali yake, baadhi ya watu wamemzoea na humchukulia kama mtu wa kawaida tu japo kwa nyakati zingine baadhi yao humuogopa hasa watoto wanapokutana naye kwa mara ya kwanza.
Alisema kuwa anafurahishwa na jamii inayomzunguka kwa kuwa humtunza kama mmoja wao na haimtengi.
“Watoto wakati mwingine ndio hunishangaa. Lakini mara nyingi huwa sikabiliwi na unyanyapaa.
Aidha alizungumzia kuhusu maisha yake ya utotoni na kusema kuwa pamoja na yote aliyokumbana nayo, huwa anayakubali kwa kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu chini ya mbingu.
“Utoto wangu ulikuwa vile vile. Watoto ni watoto tu, ni kweli walinicheka na kunichezea. Lakini nani hakufanyiwa hivyo?, sote huwa na kasoro pahala fulani. Hakuna aliyekamilika,”
Hizi ni baadhi ya picha za mwanamitindo huyo akiwa katika mionekano tofauti.
Image result for caitin stickels         Image result for caitin stickels
Image result for caitin stickels

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MFAHAMU MWANAMITINDO ANAYEUGUA ‘UGONJWA WA PAKA’
MFAHAMU MWANAMITINDO ANAYEUGUA ‘UGONJWA WA PAKA’
https://3.bp.blogspot.com/-G3FBYtInnSY/WNgIzg6bVvI/AAAAAAAAYrs/3VlcTDWLzQ8FvbOX8Lvoo_fYkcBPzysmgCLcB/s1600/xpaka-750x375.jpg.pagespeed.ic.OpbsJmkcFd.webp
https://3.bp.blogspot.com/-G3FBYtInnSY/WNgIzg6bVvI/AAAAAAAAYrs/3VlcTDWLzQ8FvbOX8Lvoo_fYkcBPzysmgCLcB/s72-c/xpaka-750x375.jpg.pagespeed.ic.OpbsJmkcFd.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/mfahamu-mwanamitindo-anayeugua-ugonjwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/mfahamu-mwanamitindo-anayeugua-ugonjwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy