MFANYABIASHARA ALIYEMPA MAKONDA SHAMBA MIKONONI MWA POLISI

Mfanyabiashara wa Kampuni ya Azimio Housing Estate ambaye hivi karibuni alimpa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ekari 1,500, Mohammed Ikbal amehojiwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma za kughushi nyaraka za serikali.
 Kuhojiwa kwa mfanyabiashara huyo kunakuja siku chache tangu alipokanusha taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwa eneo alilolitoa kwa Makonda halikuwa eneo lake bali ni mali ya Wananchi. Mfanyabiashara huyo alikanusha madai hayo huku akisema kuwa, eneo hilo ni la kwake na wala halina mgogoro kama alivyodai Waziri Lukuvi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alithibitisha kuhojiwa kwa mfanyabishara huyo jana ambapo alisema kuwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuonekana muda hautoshi kwa mahojiano, hivyo atarudi siku nyingine.
“Alikuwa na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana na anatarajiwa kuripoti siku nyingine. Anatuhumiwa kughushi nyaraka za serikali na sasa tunaendelea na uchunguzi”, alisema Kamishna Sirro.
Mfanyabaishara huyo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa, eneo alilompa Paul Makonda ni la kwake ambapo alilinunua tangu mwaka 2005. Alizidi kufafanua kuwa alinunua ekari 3,500 na kuonyesha mchango wake kwa serikali akaamua kutoa eneo hilo.
Wakati Makonda akipokea ardhi hiyo alisema ingetumika kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na maeneo ya biashara kwa ajili ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post