MKE WA KAPTENI KOMBA AMLILIA MAGUFULI

Miaka miwili imepita baada ya aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba kufariki dunia na mjane wake amejitokeza na kumuomba Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli amsaidie ili alipwe shilingi milioni 70.5 zilizobaki kama mafao ya mumewe.
Akizungumza jana nyumbani kwake Dar es salaam, Salome Komba alisema wanaidai CCM fedha hizo kutokana kazi ambazo marehemu alizokifanyia chama hicho kupitia bendi ya TOT.
“Maisha ya familia sio mazuri sana, hali imekuwa ngumu na wanangu wapo shule. Namuomba Rais Magufuli anisaidie ili nilipwe fedha za mafao ya mume wangu yatakayoniwezesha kuisimamia vizuri familia yake.
Alikuwa anaipenda sana CCM na mpaka anafariki alikuwa akiimba nyimbo za chama chake. Najua Rais ni msikivu na anajua kazi aliyoifanya mume wangu, naomba msaada ili niweze kuwaendeleza watoto.”
Alisema mpaka sasa amelipwa shilingi milioni 4.5 kati ya milioni 75 zinazodaiwa na kwamba hivi sasa anaendesha familia yake kwa ufugaji wa kuku na kwamba mafao yaliyotokana na ubunge yametumika kusomesha watoto.
Alisema madai yake ni ya muda mrefu sasa na amekuwa akiyafuatilia katika ofisi za CCM ikiwamo ya Katibu Mkuu lakini tangu kipindi hicho kiasi pekee alichopatiwa ni shilingi milioni 4.5. “Nimefuatilia mara kadhaa mafao hayo lakini sijalipwa. Mimi ni mjane, ninahitaji fedha kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo na kulea familia,” alisema Salome.
“Mbona mafao ya Ubunge tumeshalipwa? Inakuwaje haya yanachukua muda mrefu kulipwa? Ni miaka miwili sasa tangu kifo cha mume wangu kitokee. Ndiyo maana nimeamua kuzungumza na vyombo vya habari ili wanisaidie kufikisha ujumbe kwa Mwenyekiti wa chama ili nilipwe,” alimalizia Salome Komba.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post