MTU MMOJA APIGWA RISASI NA KUFA MKOANI SINGIDA

Mkazi mmoja wa Ikungi Mkoani Singida amepigwa risasi na kufa papo hapo baada ya kuwajeruhi watu wanne kwa kisu akiwemo mke wake na kuhatarisha maisha ya polisi kwa kutaka kuwachoma na kisu wakati wakitaka kumkamata.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amemtaja aliyepigwa risasi na kufariki kuwa ni Herman Joseph mkazi Ikungi madukani.
Amesema kuwa baada ya kubishana na mke wake alitoa kisu na kumchoma makalioni na watu wengine watatu walipofika kwaajili ya kutoa msaada pia aliwachoma kisu.
Aidha, Kamanda Magiligimba amesema kuwa baada ya askali kufika katika eneo la tukio Marehemu Herman alijaribu mara mbili kutaka kuwachoma kisu licha ya askali kupiga risasi hewani kumtaka ajisalimishe lakini hakufanya hivyo ndipo alipomvamia askali mmoja na kutaka kumchoma kisu.
Hata hivyo, Kamanda Magiligimba amesema kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya akili ambayo huwa yanamtokea na mara nyingine huwa anakuwa kawaida, na kuongeza kuwa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini ukweli wa tukio hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post