MTUKUTU MARIO BALOTELLI AISAIDIA NICE KUPATA SARE

Mario Balotelli amefunga goli lake la 10 katika msimu huu na kuiongoza Nice kupambana kiume ikitokea nyuma baada ya kufungwa hadi kutoa sare ya 2-2 na Caen hapo jana.

Wakati Nice ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 ikiwa zimebakia dakika 20, Balotelli alimaliza ukame wa kutofunga katika michezo minne kwa kufunga kwa shuti la karibu.

Dakika saba baadaye mchezaji aliyetokea benchi Anastasios Donis anayeichezea Nice kwa mkopo akitokea Juventus, aliachia shuti lililogonga mwamba na kutinga wavuni.
Mario Balotelli akiwa ameuchukua mpira na kukimbia nao kuuwahisha kuuweka kati baada ya kufunga goli
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post