MWANA FA AWEKA KIFUA KUILINDA HESHIMA YA PROFESA JAY

Hamisi ‘Mwana FA’ Mwinjuma amesimama kutetea heshima ya mbunge wa Mikumi Joseph ‘Profesa Jay’ Haule kwenye muziki wa kizazi kipya.
Mkali huyo wa ‘Dume Suruali’ amechukua uamuzi huo ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya Profesa kuonesha kuchukizwa na maneno yaliyoandikwa mtandaoni na Nash MC akimkosoa vikali kuhusu uamuzi wake wa kufanya Singeli.
Mwana FA ambaye ameonesha kuufuatilia kwa karibu mgongano wa mawazo na hali ya kukwaruzana mtandaoni kati ya Profesa na Nash, ameeleza kuwa sio sahihi kwa mtu yoyote kumkosoa au kumkosea heshima kwa kufanya wimbo wa aina ya ‘Singeli’ kwani ana mchango mkubwa katika muziki wa kizazi kipya.
“Mimi binafsi nina heshima ya kipekee kwa Profesa Jay,”Mwana FA aliuambia mtandao wa Bongo5. “Hakuna mtu mwenye mchango mkubwa kwenye huu muziki kama Profesa Jay. Hiyo wasiompenda wataikataa pengine, lakini mioyoni mwao watakuwa wanajua,” aliongeza.
FA alisema kuwa wimbo wa ‘Chemsha Bongo’ wa Profesa Jay ndio uliobadilisha aina na mtazamo kwa sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini na kuwashawishi hata watu wa makamu kuupenda muziki huo.
“Akija mtu mmoja ambaye hukumbuki hata wimbo wake mmoja probably, halafu akaja akamkosoa Profesa Jay kwa sababu tu amefanya wimbo wa Singeli, sio sawa,” alisema Mwana FA na kumtolea mfano rapa mkongwe wa Marekani, Snoop Doggy kuwa amekuwa akifanya hata nyimbo za reggae lakini bado heshima yake kwenye hip hop iko pale-pale.
Rapa huyo alilaani lugha iliyotumiwa na Nash MC kumkosoa Profesa Jay mtandaoni akidai kuwa ilikuwa na lengo la kumkosea heshima.
“Mimi nafikiri kama kulikuwa na mpango wa kumkosoa Profesa Jay, wangesema tu kuwa Profesa hukufanya wimbo mzuri this time. Lakini isifikie kum-disrespect (kumvunjia heshima) kuwa ‘Profesa mwenyewe ame-sale out, sijui amekuwa kama wale wanaojipanga barabarani’,” FA anakaririwa.
Alisisitiza kuwa watu wanaweza kutoa makemeo na kukosoa kwa njia ambazo hazitakuja na sura ya ukosefu wa adabu kwa msanii kama Profesa Jay.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa nahodha ya meli ya Hard Blasters Crew, Profesa Jay alifanikiwa kuwashawishi wazazi kuwaruhusu watoto wao kufanya muziki na kuongeza wasanii wengi wenye majina kwenye sanaa ya muziki wa Bongo Fleva.
Profesa Jay na Mwana FA wamewahi kushirikiana kwenye muziki ikiwa ni pamoja na kupakuwa wimbo wa pamoja wa ‘Jukumu Letu’.
Albam ya Profesa Jay ‘Machozi Jasho na Damu’ yenye nyimbo 15 inatajwa na wadau wengi wa muziki akiwemo Fid Q kuwa ndio albam bora zaidi ya muda wote ya Bongo Fleva.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post