MWANAMUZIKI SHILOLE AFUNGUKA KUHUSU KUWA MJAMZITO

Msanii filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana ujauzito wowote bali ameridhika na maisha jambo ambalo limefanya aongezeke mwili na kunenepa licha ya watu kuwa na hisia kuwa huenda ana ujauzito.
Shilole amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa kumi na mbili kamili.
“Mimi saizi sina ujauzito wowote sema nimenenepa tu maana nimeridhika na maisha haya haya, ukimya wangu ni kwa sababu nilikuwa nazipa ngoma nafasi saizi nimeamua kuja rasmi na wimbo wangu huu ‘sitoi kiki’ kwani nimegundua Watanzania wanataka burudani, saizi pesa hakuna hivyo nimeona bora nije kuwaliwaza na muziki mzuri huu” alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole amesema video ya wimbo huo ataifanya na waongozaji kutoka hapa hapa Tanzania.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post