MWENYEKITI WA CCM, DKT MAGUFULI ATEUA VIONGOZI WAPYA LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mpainduzi CCM, Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho mkoani Dodoma leo ameteua viongozi wapya watatu ambapo waliokuwa wakishikilia nafasi hizo sasa watapumzika.
Dkt Magufuli ametaja majina hayo wakati akifunga mkutano huo uliokuwa wa kuidhinisha mabadiliko yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) iliyokutana Disemba mwaka jana, Ikulu jijini Dar es Salaam. Majina hayo ya viongozi wapya watatu wa CCM yamepitishwa kwa kauli moja na wajumbe wa mkutano mkuu.
Viongozi hao wapya walioteuliwa ni  Dk. Abdallah Juma Abdallah, ambaye atakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Perreira Silima ambaye atakuwa Katibu wa Oganaizesheni na Dk. Frank Haule ambaye atakuwa Katibu wa Uchumi na Fedha akichukua nafasi ya Mama Zakia Meghji.
Chama cha Mapinduzi kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake mbalimbali mwaka huu baada ya viongozi waliopo kumaliza muda wao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post