NAHODHA NA KOCHA WA ZAMANI WA LIVERPOOL AFARIKI DUNIA

Nahodha na Kocha wa zamani Liverpool Ronnie Moran amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83.

Moran alichezea klabu hiyo mechi 379 kati ya 1952 na 1966 na alikuwa mfanyakazi aliyehudumia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi alipostaafu 1999.

Alijiunga na benchi la wakufunzi Liverpool mwaka 1966 na mara mbili alihudumu kama meneja wa muda – baada ya Kenny Dalglish kujiuzulu 1991 na Graeme Souness alipofanyiwa upasuaji wa moyo 1992.

Mwanawe wa kiume amethibitisha kwamba alifariki mapema Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Alihudumu chini ya mameneja tisa tofauti alipokuwa benchi la kiufundi.

Aliwaongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA wanjani Wembley mwaka 1992 akiwa meneja wa muda meneja wao Souness alipokuwa anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post