NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA SADC WA KUJADILI MASUALA YA USALAMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) (hawapo pichani), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto meza kuu) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga, na kulia ni Afisa wa kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Rokhayatou Diarra. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wapili kulia meza kuu) akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia meza kuu ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye pia alifungua mkutano huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisindikizwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (kulia), mara baada ya Masauni kufungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo ambapo Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo walijadili masuala mbalimbali ya usalama. Warsha hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wanne kulia), Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo mara baada ya Masauni kuufungua Warsha hiyo iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo. Warsha hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post